KINANA: CCM HAIWEZI KURUBUNIWA KWA SABABU YA KUPATA KURA

 Balozi Hilda Komba wa shina namba 9 Tawi la Amani Makolo akimkaribisha nyumbani kwake Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na wanachama wa shina namba 9,katika tawi la Amani Makolo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Aman Makolo waliojitokeza nyumbani kwa Balozi Hilda Komba wa shina namba 9 ,Tawi la Amani Makolo wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma.
 Wanachama wapya wa Tawi la Amani Makolo wilayani Mbinga wakila Kiapo cha Uanachama wa CCM mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  ambaye leo amefanya ziara katika wilaya ya Mbinga.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa Shina namba 9 Tawi la  Amani Makolo ambapo aliwapongeza kwa ushirikiano na mshikamano waliokuwa nao kiasi wameweza kuwa na wanachama hai 426.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Mtundawalo wakati akiwasili kijijini hapo tayari kwa kufanya mkutano wa hadhara.Katika Mkutano wa hadhara Katibu Mkuu wa CCM alizungumzia mipango mbali mbali ya kutatua matatizo ya wananchi na kuwaeleza wananchi CCM haiwezi kurubuniwa  kwa sababu ya kupata kura,akasisitiza wananchi wawe wa kweli kwa serikali ili haki itendeke kwa haraka.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na viongozi wengine wa CCM kulima shamba la wanawake na vijana wajasiriamali Mkwaya kata ya Kilimani.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajasiriamali wa Mkwaya kata ya Kilimani ambao kwa pamoja wameamua kujishughulisha na kilimo.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akiwasalimu wakulima wa kata ya Mkwaya .
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ngoma ya Mganda wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano wilayani Mbinga.

 Katibu wa NEC Itikadi na uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mbinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya michezo Mbinga mjni.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kukabidhi pikipiki 50 zilizotolewa na mbunge kwenda kwa watendaji wa vijijini.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimueleza Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose uzoefu wake wa kuendesha  pikipiki,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga  Ndugu Senyi Ngaga.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Mbinga mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanika kwenye viwanja vya michezo vya Mbinga mjini ambapo aliwaeleza wananchi kuwa chama cha Mapinduzi kitasaidia kutoa ushauri kwa mazao ambayo bei yake inashuka na kupanda.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa Wilaya wa zamani Ndugu Osmund Kapinga.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Mzee Osmund Kapinga Mkuu wa Wilaya mstaafu mara baada ya kukamilika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya michezo  vya Mbinga mjini mkoa wa Ruvuma.

No comments:

Post a Comment