KINANA AITEKA BOMBA MBILI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa wilaya ya Songea mjini wakati akiwasili viwanja vya Bombambili tayari kuhutubia wananchi wa wilaya hiyo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia umati wa watu waliofurika katika viwanja vya Bombambili wilaya ya Songea mjini ambao aliwaambia wananchi hao kuna haja ya hatua za haraka kuchukuliwa kwa watendaji wa serikali ambao si wasikivu na hawapo tayari kutatua matatizo ya wananchi.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho akiwasalimia wakazi wa wilaya ya Songea mjini kabla ya  kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuhutubia wananchi wa Songea mjini kwenye viwanja vya Bombambili.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa wilaya ya Songea mjini ambapo aliwaambia wananchi maendeleo yanakuja hatua kwa hatua na amewataka watumishi wa serikali kufanya kazi za wananchi,Katibu Mkuu pia alitumia fursa hiyo kuzungumzia mambo mbali mbali yanayoleta mkingamo kwenye mchakato wa kupata Katiba Mpya na kusema "Katiba mpya si suluhu ya maendeleo yetu".
Wananchi wa wilaya ya Songea mjini wakimuaga Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Bombambili wilayani Songea mjini mkoa wa Ruvuma.

No comments:

Post a Comment