KINANA AANZA ZIARA WILAYA YA SONGEA MJINI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali wa CCM waliofika kumlaki alipowasili kwenye eneo maarufu linalojulikana kama Nonga Nonga wilaya ya Songea mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abrahman Kinana akishiriki shughuli za ujenzi katika Zahanati ya Mahilo wilayani Songea mjini .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na waasisi wa CCM wilaya ya Songea mjini, kutoka kushoto ni Mzee Hashimu Gawaza na kulia kwa Katibu Mkuu ni Mzee Clemenci Nyoni ambao walikaa kikao cha kwanza na Mwalimu Nyerere tarehe 12 Agosti 1957 wakati wa harakati za kuikomboa nchi,anayefuatia kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wazee waasisi pamoja na wananchi wa kata ya Matogoro ambapo alitaka wana CCM kuenzi kazi zilizofanywa na waasisi wetu kwa kudumisha mshikamano ,umoja na amani.
 Ofisi ya Kata ya Matogoro  CCM ambayo iliwekwa jiwe la msingi tarehe 20 Desemba 1986 na Mzee Rashid Mfaume Kawawa,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ameahidi kutoa bati za kuezeka ofisi  hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchama wa Shina namba 1tawi la Ambachai kata ya Mfaranyaki nyumbani kwa Balozi wa Shina Ndugu Magreth Mchula,Katibu Mkuu alisisitiza viongozi wa ngazi za chama kuwa na mazoea ya kutembelea mabalozi wao kwani ndio msingi wa wanachama.
 
 Wanachama wa Shina namba 1 wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,pichani Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa amejumuika na wanachama kukaa nao pamoja kwenye mkeka.

 Mzee Mustafa Mohamed Songambele akionyesha furaha yake alipokutana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana , Mfaranyaki Songea,Katibu Mkuu ameanza leo ziara ya kuetembelea wilaya ya Songea mjini.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimiana na Mzee Mustafa Songambele mmoja wa waasisi wa Tanu na mwanasiasa wa muda mrefu.
 Mlevi wa Vijana wajasiriamali wa Mfaranyaki Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimu vijana hao baada ya kufunguliwa kwa Shina lao na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ngoma ya kutoka kikundi cha ngoma cha Mfaranyaki baada ya kuzindua shina la vijana wajasiriamali wa Mfaranyaki.


No comments:

Post a Comment