ZIARA YA KINANA SHINYANGA VIJIJINI YAFANA SANA

Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika wilaya ya Shinyanga vijijini imekuwa na mafanikio makubwa sana. Katibu Mkuu ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye.

Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu aliweza kushiriki katika ujenzi wa Birika la kunyweshea maji Mifugo  na kutembelea mradi wa soko jipya la kisasa katika kata ya Didia, pia Katibu Mkuu alitembelea mradi wa ujenzi wa Hospitali katika kata ya Iselamagazi.

Katibu Mkuu pia allihtubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Salawe na kisha kufanya kikao na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM ngazi ya Wilaya na kumalizia kwa kukutana na Wazee wa Kata ya Iselamagazi.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa Birika la kunyweshea maji mifugo katika kata ya Didia.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na mafundi wanaoshiriki kujenga Birika la kisasa la kunyweshea maji mifugo katika kata ya Didia.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa soko la kisasa katika kata ya Didia wilaya ya Shinyanga Vijijini, tarehe 11 Septemba 2013.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitembelea mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya katika kata ya Iselamagazi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Ndugu Juma Mayenze mkazi wa kijiji cha Mwabenda kata ya Solwa ambaye alikuwa anawakilisha kilio cha wakazi wa kijiji hicho juu ya lini watapata maji na umeme.
 'JEMBE LA CHAMA haogopi chochote ulimwenguni' Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimbeba nyoka aina ya chatu nje ya jengo la soko jipya na la kisasa lililopo kata ya Didia,Shinyanga Vijijini.
 Katibu Mkuu akiangalia moja ya sanaa za kundi la msanii Tangawizi Elias kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara katika viwanja vya Salawe.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Salawe wilaya ya Shinyanga Vijijini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika tarehe 11 Septemba 2013 kwenye viwanja vya Salawe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya Salawe wilaya ya Shinyanga Vijijini .
 Mbunge wa Viti maalum Azah Hilal Hamad akihutubia wakazi wa Salawe ,wilaya ya Shinyanga Vijijini ambapo mbunge huyo alimuomba Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana awasaidie kusukuma masuala ya maji,umeme na huduma ya afya.
 Wananchi wakisikiliza hotuba za viongozi wao kwa makini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Salawe.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiwaaga wajumbe wa halmashauri ya CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini mara baada ya kumalizika kwa kikao.

No comments:

Post a Comment