ZIARA YA KINANA BUTIAMA


Mapokezi  ya Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana  katika wilaya ya Butiama Mkoani Mara.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikaribishwa wilaya ya Butiama na Mkuu wa wilaya hiyo Angeline Mabula
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi waliokuja kumpokea wakati anawasili kwenye wilaya ya Butiama.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa heshima katika kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na mtoto wa kwanza wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage anayefahamika kwa jina la Andrew nyumbani kwa Baba wa Taifa Butiama,kushoto pichani ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  Nape Nnauye.


Katibu Mkuu wa CCM Taifa akisalimiana na mdogo wa Mwalimu Nyerere ,Daniel Nyerere walipokutana kwenye kikao cha Balozi wa shina namba 12 tawi la Butiama.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na mdogo wa Mwalimu Nyerere ,Daniel Nyerere walipokutana kwenye kikao cha Balozi wa shina namba 12 tawi la Butiama.
 
Bibi Safina Kombo balozi mstaafu akielezea matatizo yanayowapata wajane kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipotembelea shina namba 12 tawi la Butiama

Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Zahanati ya kata ya Busegwe.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na wazee wa kabila la Wazanaki
 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Chifu Ihunyo iliyopo Busegwe wilaya ya Butiama.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiwa ameshikilia maru maru (tiles) pamoja na Mbunge wa jimbo la Butiama vijijini Ndugu Nimrod Mkono ambapo mbunge huyo amejitolea bati zaidi ya mia tatu pamoja na tiles na milango yote.

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndugu Amina Makilagi akihutubia wakazi wa Kyabari wilaya ya Butiama na kuwaasa juu ya mauaji yanayoendelea ya akina mama na kuwataka waache mara moja kwani inawachafulia sifa Mkoa wa Mara.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kyabari, wilaya ya Butiama na kuwaambia wawe makini na vibaraka wanaotumika kutaka kuvuruga umoja na mshikamano wetu kwa kupitia mchakato wa Katiba.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipewa heshima ya Mzee wa Kizanaki kutoka kwa wazee wa kabila la Kizanaki .
 Kikundi cha Ngoma cha Egumba wakicheza ngoma ya Dilandi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Kyabakari na kuhutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Kyabakari wilayani Butiama na kuwaambia ni muhimu kuzingatia misingi iliyojegwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hasa katika suala zima la Ujamaa,Kujitegemea na Maadili.
 No comments:

Post a Comment