KINANA: MAWAZIRI TATUENI KERO ZA WANANCHI


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakazi wa kata ya Mwandoya ,kijiji cha Mandoya tarafa ya Kisesa ambapo Katibu Mkuu alipata maelezo ya utekelezaji wa ilani ya CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia maendeleo ya hatua za awali za ujenzi wa daraja la Mongobakama ambalo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM akipokelewa na umati wa wakazi wa kijiji cha Mwasengela ambao kwa ni nadra kupata viongozi wa kitaifa kwenye kijiji chao.
 Mkuu wa Wilaya ya Meatu Rosemary Kirigini akisalimia wakazi wa kata ya Mwasengela wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alihutubia.
 Mbunge wa Kisesa Ndugu Luhaga Mpina akihutubia wakazi ya kata ya Mwasengela kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni wa heshima alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wakazi wa kata ya Mwasengela ambapo yupo kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mkoani   Simiyu .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na aliyekuwa mgombea wa udiwani kwa tiketi ya TLP lakini sasa amejiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi Zunzu Ndatulu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mwasengela.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Mwangesela wilayani Meatu mkoani Simiyu ambapo aliwasifu wakazi wa kata hiyo kwa kuichagua CCM na kupata viongozi wanaoleta maendeleo.
 :Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina akiwatambulisha wazazi wake kwenye mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia wananchi ilimchukua miezi mitatu kukubaliwa kwa ombi lake la kutaka kugombea ubunge jimboni kwake.
 Chifu Kilabanja Abdulrahman Kinana akiwaaga wakazi wa kata ya Mwasengela baada ya kumaliza Mkutano wa hadhara.
Sehemu ya umati uliofika kwenye mkutano wa hadhara kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya mikoa mitatu ambapo kwa sasa yupo mkoani Simiyu na atamalizia mkoa wa Mara, tayari Katibu Mkuu ameshamaliza ziara ya mkoa wa Shinyanga na kuleta neema kwa wakulima wa pamba na wafugaji.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na mbunge wa Kisesa Ndugu Luhaga Mpina na wazazi wa mbunge huyo mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amewataka mawaziri husika kutatua kero za wananchi baada ya watendaji wa chini kushindwa kufanya kazi zao, alisema sasa baadhi ya watendaji wamegeuza kero za wananchi mitaji  na kuwachajisha pesa nyingi hasa wafugaji.
Akihutubia wakazi wa kata ya Mwasengela alisema mawaziri lazima wachukue jukumu la moja kwa moja kutatua matatizo ya wananchi, alisema wafugaji wa kata ya Mwasengela wamekuwa wakibughudhiwa na watu wa hifadhi ya Maswa  kupita kiasi, alisema sheria zingine ziangalia wakati zinaweza zikawa zimepitwa na wakati hivyo ni vyema zikarekebishwa.

No comments:

Post a Comment