JUMUIYA YA WAZAZI (CCM) WILAYA YA ILALA WAIPONGEZA MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI KWA UTEKELEZAJI MKUBWA WA MAJUKUMU YAKE.


 Wajumbe wa Jumuiya ya wazazi wakipata maelezo ya umuhimu wa matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa kwa sekta ya kilimo na mifugo kutoka kwa Meneja huduma za hali ya hewa- kilimo Bw. Isack Yonah (Hayupo pichani)
Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Ilala wakipata maelezo jinsi ya kurekodi utabiri wa kila siku katika studio ya TMA iliyopo katika ofisi za Mamlaka- Makao Makuu, Ubungo Plaza
Meneja wa ofisi ya utabiri Bw. Samwel Mbuya akitoa maelezo jinsi mchakato wa uandaaji utabiri unavyofanyika wakati wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Ilala walipotembelea ofisi hizo.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt. Agnes Kijazi ( wa pili kulia waliokaa) akifuatiwa na mwakilishi wa mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Ilala Bi. Angelina Malembeka  katika picha ya pamoja na wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi na uongozi wa TMA.



JUMUIYA YA WAZAZI (CCM) WILAYA YA ILALA WAIPONGEZA MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI KWA UTEKELEZAJI MKUBWA WA MAJUKUMU YAKE.

Jumuiya ya Wazazi (CCM) Wilaya ya Ilala imetembelea ofisi za Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini ili kujifunza shughuli mbali mbali zinazofanywa na  Mamlaka ikiwemo utayarishaji wa utabiri na usambazaji wake husasan taarifa za hali mbaya ya hewa. 

  Katika msimu wa MASIKA  uliomalizika mwezi Mei mwaka huu maeneo mengi ya Wilaya ya Ilala yaliathirika na mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha katika maeneo mengi nchini. Aidha wajumbe wa Jumuiya waliipongeza TMA kwa kufanikisha kutoa tahadhari kwa wakati hivyo kupunguza madhara ya vifo kwa wananchi waishio maeneo hatarishi na kuahidi kushirikiana na Mamlaka katika kusambaza taarifa za hali ya hewa kwa wananchi wote hasa wa Jiji la Dar es Salaam. 

    Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Ilala iliongozwa na  Bi Angelina Malembeka (Diwani wa Msongola) aliyemuwakilisha Mwenyekiti wa Jumuiya, Katibu wake Bw. Lugano Mwafonga, diwani wa Kariakoo Bw. Abdulkarim S. Masamaki , wenyeviti na makatibu kata wa Wilaya ya ilala ambapo ujumbe huu ulipokelewa na Mkurugenzi  Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi na menejiment yake.


No comments:

Post a Comment