BENKI YA DUNIA: UCHUMI UMEKUWA LAKINI NAFASI FINYU ZA AJIRA



 Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda akizungumza na waandishi wa habari  nje ya Hotel ya Serena ambapo alihudhuria Mkutano wa Tano unaohusu masuala ya Uchumi,kulia kwake ni mkurugenzi wa benki ya Dunia nchini Ndugu Philippe Dongier
 Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Philippe Dongier akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa kivukoni Serena Hotel jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na Mwandishi wa Mada Ndugu Jacques Morisset ambapo aliwaeleza waandishi hao Tanzania ina nafasi kubwa ya kupanua wigo wa ajira kwa kutengeneza mazingira ya kufanyia kazi yenye ubora hasa kwenye  miji inayokuwa kwa kasi hii itasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa Vijana na Wanawake.
 Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Philippe Dongier akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa kivukoni Serena Hotel jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na Mwandishi wa Mada Ndugu Jacques Morisset ambapo alikiri pamoja na kukua kwa uchumi lakini bado uchumi haujafungua au kutengeneza ajira kwa wananchi .
(Picha na Adam Mzee). 

MANGULA AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA CHINA



 Viongozi wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa  China Li Yuanchao(hayupo pichani) kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Philip Mangula akimkabidhi zawadi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa  China Li Yuanchao mara baada ya kumaliza mkutano .
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa  China Li Yuanchao akionyesha zawadi aliyopewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula mara baada ya kumaliza mkutano baina ya viongozi wawili.
 Balozi wa China Nchini Tanzania Lu Youqing akifafanua jambo wakati wa Semina ya Ujamaa iliyohusisha CCM na CPC kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula akizungumza wakati wa Semina inayohusu Umuhimu wa Ujamaa na Kukua kwa Uchumi,wengine pichani(kushoto) ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Abdala Bulembo ,Mwakamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Mboni Mhita ,Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM Ndugu Sixtus Mapunda ,Profesa Max Muya ,na Makwaia wa Kuhenga.
 Mr Ma Zhongji kutoka Ubalozi wa China akisaidia kutafsiri wakati wa Semina ya Ujamaa iliyohusisha CCM na CPC iliyofanyika kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa kutoka CCM Makao Makuu wakifuatilia kwa makini Semina inayohusu Umuhimu wa Ujamaa katika Kukua kwa Uchumi iliyofanyika katika ukumbi wa Kivukoni,Serena Hotel Dar es Salam.
 Mheshimiwa Kingunge Ngombale Mwiru akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Hotel ya Serena jijini Dar Es Salaam  na kuwaeleza kuwa Watu wanajenga Ujamaa wenyewe haujengwi na Viongozi peke yao.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kukamilika kwa Semina inayohusu Ujamaa iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo Mangula liwaeleza waandishi hao kuwa Ujamaa unatakiwa Ueleweke,Utekelezwe na Uendelezwe,Semina hiyo iliwahusisha vyama vya CCM na CPC kutoka China.

WARSHA YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UANDISHI WA HABARI ZA KITAKWIMU YAFANYIKA MKOANI MOROGORO



Mkurugenzi wa Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morice Oyuke (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Morogoro leo wakati akifungua Warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu namna bora ya kuandika habari za kitakwimu. Kulia ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa.
Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa (kulia), akitoa mada katika warsha hiyo. Kushoto ni Watakwimu, Stephano Cosmas na Hashim Njowele.
Mkurugenzi wa Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morice Oyuke (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Morogoro leo wakati akifungua Warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu namna bora ya kuandika habari za kitakwimu. Kulia ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa.
Mtakwimu, Stephano Cosmas, akitoa mada katika warsha hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo.
Maofisa wa Takwimu, Stephano Cosmas na Hashim NNjowele wakisubiri kutoa mada katika warsha hiyo.
Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa (kulia), akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morice Oyuke (kushoto), kufungua warsha hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk.Albina Chuwa.
Wanahabari wakiwa katika warsha hiyo.
Dotto Mwaibale, Morogoro
WAANDISHI wa Habari nchini wametakiwa kutumia taaluma yao kwa ajili ya kuhamasisha Umma kuhusu umuhimu wa Takwimu.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Takwimu za Kiuchumi Morice Oyuke kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.mjini Morogoro leo asubuhi wakati akifungua Warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu namna bora ya kuandika habari za kitakwimu.
"Ninyi wanahabari ni muhimu katika masuala ya takwimu hivyo ni vizuri mjifunze jinsi takwimu zinavyoisaidia serikali, wadau wa maendeleo na wadau wa takwimu katika kupanga Sera na kufanya tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kama vile Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 Tanzania Bara na mwaka 2020 Tanzania Zanzibar" alisema Oyuke.
Oyuke alitaja mambo mengine wanayopaswa kujifunza ni Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania Bara (Mkukuta) Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar (Mkuza) na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2010/11 mpaka 2015/16 na Malengo ya Melenia (MDGs)
Alisema eneo jingine watakalofundishwa ni kuhusu Pato la Taifa na jinsi linavyokokotolewa na bei za ajira, takwimu za jamii na umuhimu wake.
Dk.Chuwa alisema vyombo vya habari vinajukumu la kutoa taarifa sahihi zilizo rasmi ambazo zinazalishwa na tafiti mbalimbali nchini ili ziwafikie wadau wote nchini bila ya kupoteza maana.

SKYLIGHT BAND YAZIDI KUKUBALIKA NA MASHABIKI, LEO KUZINDUA WIMBO WAO MPYA "PASUA TWENDE" NDANI YAK IOTA CHA THAI VILLAGE


Vijana machachari wa Skylight Band Kutoka kushoto Donode, Digna Mbepera, Sony Masamba na Mary Lucos wakitoa Burudani kwa mashabiki wao ndani ya Thai Village,USikose Leo kutakuwa pia na Uzinduzi wa Wimbo wao mpya PASUA TWENDE Itakuwa hapatoshiii.

Weweeee Usicheze na Sony masamba(katikati)akiyarudi mauno safi kabisaaaa kuwapa burudani wapenzi wa Skylight ndani ya Thai Village.

Hapo hapooo Taratibuuuu weweee Sam Mapenzi akiyarudi mastep ndani ya Thai Village Sony Masamba akifuahiii na Mashabiki Wake.

Sony Masamba (Mutoto ya kongo)akiporomosha Vocal Kali Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha maraha Thai Village.

Kijana mdogo lakini mwenye Vocal kali : Hashim Donode akiimba kwa hisia kali kabisaaaa Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha maraha Thai village Sogea leo upate nyimboo kali pamoja na Uzinduzi wa Wimbo wao mpya.

Digna Mbepera (katikati)akifurahiii kwa staili kaliii za kuzungusha zungusha kwenye steji.

Hatariiiii hebu yaone majembe ya Skylight Band wakiongozwa na Joniko Flower(kushoto)Sony Masamba(katikati)na Sam mapenzi wakicheza sebene kaliiii za nguvuuu.

Hahahhaah Hapo sasaaaa hebu ona uchezaji wa staili hizooo ni Shidarrrrrrrrr

Sasa Hebu Tazama Iyo Video Hapo Chiniii Uamini ninachokuelezea Kutoka kwa Vijana Hawa mahiri wa Skylight Band.

DSC_0073

Daudi Tumba akifanya yake kwenye Tumba zake.

DSC_0085

Mpiga kinanda mahiri wa Skylight Band akikung'uta nota za kinanda ipasavyooo,Kwa mbaliii mzee wa drums Idrisa akizicharangaaaa drums zakeee.

DSC_0096

Mpiga Solo Gitaaa Allen Kisso akicharaza nyuzi zake 6 kwa Umahiri mkubwa kabisaa yani Rahaaa sanaaaa ukiwa unapewa burudani na Vijana hawa Ndani ya Thai Village

DSC_0160

Mpiga Bass Gitaa wa Skylight Band Tophy bass akilisukuma gita lake kwa umahiri kabisa.

Huyo ni Sam Mapenzi bwana au Tamu ya warembo akitoa vocal Kaliiiii kwa mashabiki wake.

Hahahahah Back Stage Napo Paliwaka Motoooooo wakati Donode na kampani yake wakiyarudi Mangoma kwa raha zaooooo.

DSC_0150

Huyo anaitwa Dr. Sebastian Ndege (Jembe ni Jembe) Mmiliki wa Bendi ya Skylight akimpa maelekezo kijana wake Sam Mapenzi kuhusiana na Uzinduzi wa wimbo wao mpya Ijumaa ya Leo Ndani ya Thai Village Usikoseeeeee.

Haya Sasa mashabki haoooo wakipata kitu roho inapenda

DSC_0083

Heehehehehe Ayeeeee Ayeeeeeeeee mashabiki wakiimba wimbo wa Davido sambamba na Vijana wa Skylight Band (hawapo pichani)

Weweeeee acha kabisaaaaa ni raha sana unapokuwa ndani ya Thai Village na Skylight Band usikose Ijumaa ya leoooo

Hapo sasa Diva wa Skylight Band Digna Mbepera akiwaongoza wenzake kutoa burudani kaliiii ndani ya Thai Village

DSC_0088

DSC_0090

Mary Lucos(katikati)akitoa burudani akipewa sapoti na Sony Masamba na wengine.

Hapoooo Hapoooo zungushaaa zungushaaaaa vijana wakiyarudi mauno kwa staili kaliiiiii

Weweeeee sio kwamba Viuno Vinauma Hapanaaaaa Bali ni staili ya kucheza hiyooooo hahaha njooo njoooo na wewe Ijumaaa ya leo Uchezeeee usuuze rohoo

DSC_0101

Mary Lucos akifurahiiii kuona mashabiki wake wanafurahia burudani kaliiii kutoka kwaooooo.

Back Stage Sasaaaa Ni Mda wa Ukodakkkk Hapo ni Donode na Digna Mbepera.

Mdau mkubwa Sana wa Skylight band Zainul Mzige akipata Ukodak na Mary Lucos ndani ya Thai Village unapenda kupiga pichaaaaa?Njoo Thai Village Ijumaa Ya Leo

Wadau wakubwa wa Skylight Band wakipata Ukodak wa nguvuuu.

Mdau Zainul Mzige akiwa na mdau mwenzake wa Skylight Band.

Huyu ndio Mbunge mtarajiwa wa Vunjo Bwana Sillas Mbuya akipata ukodak.

DSC_0159

Hahahaha Huyo Ndio Jembe ni Jembe (Dr. Sebastian Ndege) akifurahia Muziki mzuriiiiiiiiii wa Vijana wake ndani ya Thai Village

Mashabiki kwa rahaaaaaa zaooooo.

Ohhhhhh Mama weee Hapo ni shabiki kapata Mzukaaaa wa kutosha akaamua kumuonysha Sam Mapenzi what she got it from her mama yaniiiii kiunooooooooo

Ona raha hizooooo...Hazipo kwingineeee bali ni Skylight Band pekeeeee njooo Ijumaaaa Ya Leoo upate raha ya kutoshaaaaaaa.

DSC_0135

Nyomiiiiii la kutoshaaaaa wakifurahiaaaa muziki mzuriiiiiiiii

Mamaaaaa Weee Huo ni mduaraaaa unaitwaaa...wanasema mwanamke nyongaaaa haya sasa Tazama nyonga hizoooo.

DSC_0154

Mary Lucos akaamua kwenda kucheza na shabiki wake kwa raha zaoooo

Ehhhh raha ya mduaraaaa ni kuzungusha duara na Viunooo nyorotiiiiiiii,sasa ona mambo hayooooo

Usikose Ijumaa Ya leo kutakuwa na Uzinduzi wa Wimbo mpya wa Skylight Band pamoja na masuprizeeeee kibaooooooooo ndani ya Thai Village kuanzia saa tatu kamiliiii Usikoseeeeeee