RAIS KIKWETE KUHUDHURIA MKUTANO WA 23 WA UMOJA WA AFRIKA


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Malabo, Equatorial Guinea, leo Juni 24, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Equatorial Guinea Mhe Vicente Ehate Tomi alipowasili  katika katika uwanja wa ndege wa Malabo, Equatorial Guinea, Juni 24, 2014

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mji mkuu wa Equatorial Guinea wa Malabo  Juni 24, 2014 kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa Africa – African Union (AU).
Akiwa Malabo, Mheshimiwa Rais Kikwete pia atakuwa Mwenyekiti wa kikao cha wakuu wa nchi wanachama wa AU kitakachojadili mazingira. Rais Kikwete na ujumbe wake anatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa wiki.


No comments:

Post a Comment